Wasifu(kwa ufupi)Dwayne Johnson Douglas alizaliwa Hayward, California Mei 2, 1972 na Rocky Johnson(baba) na Ata Johnson(mama) . Alipokuwa akikua, Dwayne alisafiri sehemu nyingi na wazazi wake na kuangalia baba yake alivofanya katika ulingo.
Katika miaka yake ya shule ya sekondari, Dwayne alianza kucheza mpira wa miguu na baadae alipata udhamini kamili kutoka Chuo Kikuu cha Miami ambako alikuwa na mafanikio makubwa kama mchezaji mpira wa miguu.
Mwaka 1995, Dwayne alipata mateso ya kuumia mgongo ambayo yalimfanya kukosa nafasi katika NFL. kisha baadae akasaini mkataba wa miaka 3 na Ligi ya Canada lakini aliondoka baada ya mwaka mmoja ili kutekeleza kazi katika mieleka.
Dwayne alifanya mieleka yake ya kwanza katika USWA chini ya jina Flex Kavanah ambapo alishinda michuano ya timu tag na Brett Sawyer. Mwaka 1996, Dwayne alijiunga na WWE akitumia jina la Rocky Maivia ambapo alijiunga na kundi lililojulikana kama "The Nation of Domination".
Rocky hatimaye alichukua nafasi ya juu ya uongozi wa "The Nation of Domination" na kuanza kuchukua persona ya The Rock. Baada ya mgawanyiko "The Nation of Domination", The Rock alijiunga na kundi liingine la wasomi wa mieleka linalojulikana kama "Corporation" na kuanza feud kukumbukwa na Steve Austin.
Lakini baadae Rock alitolewa nje ya "Corporation". Akaanza kujitegemea na kujulikana kama "The Peoples Champion". Mwaka 2000, Rock alichukua muda nje ya WWE na kuanza kufanya filamu ,muonekano wake katika Mummy Returns (2001). Alirudi mwaka 2001 wakati wa uvamizi wa WCW / ECW ambapo alijiunga na timu ya wrestlers WWE The Scorpion King(2002), prequel Mummy Returns (2001).








0 Comments