habari

header ads

#Jinsi Ya Kutengeneza Chapati Za Kusukuma



Unga kilo moja weka sukari kijiko kimoja cha chai pamoja na chumvi kijiko kimoja cha chai

weka mafuta ya kupikia yamoto kikombe kimoja cha chai kidogo kisha changanya

Kisha weka maji ya uvugu vugu kikombe kimoja cha chai kidogo na endelea kuchanganya

Kanda mpaka upate mchanganyiko mzuri laini na mkavu

Kata saizi ya unga ambao ukisukuma itatosha kwenye kikaango chako

huu ni muonekano wa chapati ndogo itakayoweza kuenea katika kikaango kidogo hata kwa matumizi ya nyumbani iweke kwenye kikaango cha moto bila mafuta pika pande zote mbili

kisha weka mafuta naigeuze geuze

hii ni chapati yako imekamilika na ni laini na ina lea kama daftari na ni tamu kupita maelezo

Post a Comment

0 Comments